EPL

O’Hara ataka Spurs imfute kazi Igor

LONDON: England

ALIYEKUWA kiungo wa Tottenham Hotspur ‘Spurs’, Jamie O’Hara, amemtaka uongozi wa klabu hiyo kumfuta kazi kocha Igor Tudor kufuatia kipigo kikubwa cha mabao 5-2 dhidi ya Atlético Madrid katika mchezo wa UEFA Champions League.

O’Hara, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa redio ya talkSPORT, alionesha kukerwa na kiwango cha Tottenham Hotspur baada ya timu hiyo kufungwa nchini Hispania, akidai kocha huyo wa muda hafai kuendelea kuinoa timu hiyo ya London Kaskazini.

Akizungumza katika kipindi cha Sports Bar, O’Hara amesema haamini alichokiona uwanjani na kudai Spurs imepoteza mwelekeo wake.

“Nini kinaendelea? Spurs wamefanya tena makosa yale yale. Hii ni aibu kabisa. Kocha huyu lazima aondoke sasa. Afukuzwe,” amesema O’Hara.

Hata hivyo, kauli zake zilizua mjadala mkali studio baada ya mtangazaji mwenzake na mchezaji wa zamani wa Chelsea FC, Jason Cundy, kumkejeli kwa kuvaa barakoa ya aliyekuwa kocha wa Spurs Ange Postecoglou huku akicheka.

Cundy pia alitumia kauli ya kejeli akibadilisha kauli mbiu ya Spurs “To Dare Is To Do” na kuwa “To Dare Is To Poo”, jambo lililomkera zaidi O’Hara hadi kuamua kutoka studio kwa hasira.

Kocha Tudor aliteuliwa kuinoa Spurs kwa muda takribani siku 26 zilizopita, lakini kipigo hicho kizito kimeongeza presha kwa uongozi wa klabu hiyo huku mustakabali wake ukizidi kuwa mashakani.

Related Articles

Back to top button