Loemba akabidhiwa gari, wengine kufuata

DAR ES SALAAM : KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Inno Loemba, amekabidhiwa gari aina ya Toyota Crown New Model na kampuni ya Jayerutty Investment moja ya wadhamini wa klabu hiyo.
Loemba ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliosajiliwa kwa ushirikiano na kampuni hiyo, kufuatia makubaliano ya kimkataba kati yao na Simba SC ambayo yanaitaka kusaidia usajili wa angalau mchezaji mmoja kila msimu.
Mbali na Loemba, kampuni hiyo pia imetangaza kuwa itawakabidhi magari wachezaji wengine watatu ambao ni Libasse Gueye, Anicet Oura, na Djibrilla Kassali mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gari hilo leo Mkurugenzi wa kampuni hiyo CPA Joseph Rwegasira amesema kuwa lengo la hatua hiyo ni kuongeza thamani kwa wachezaji na kuwapa motisha zaidi.
“Hii ni motisha kwa wachezaji wetu ili waweze kufanya vizuri zaidi katika michezo yote na kufikia malengo ya timu,” amesema Rwegasira.
Mwisho




