Nyumbani
FIFA yaifungia Simba kusajili
SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Mguu(FIFA) limeifungia klabu ya Simba kusajili mpaka itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mchezaji Pape Ousmane Sakho.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Mguu Tanzania(TFF) imesema uamuzi umefanywa na FIFA baada ya Teungueth kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho.
“Simba ilitakiwa iwe imetekeleza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa lakini haikufanya hivyo,”imesema taarifa hiyo.
Wakati FIFA imeifungia Simba kufanya uhamisho wa wachezaji wa kimataifa, TFF imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa ndani.
Kabla ya kujiunga na Simba, Sakho ambaye hivi sasa anacheza timu ya Quevilly Rouen Metropole ya Ufaransa alikuwa mchezaji wa Simba.