Ligi Kuu

Singida BS yamrejesha kundini Aucho

SINGIDA: KLABU ya Singida Black Stars imetangaza kumsamehe na kumrejesha kundini kiungo wake Khalid Aucho.

Awali, klabu hiyo ilitangaza kumfungia mchezaji huyo miezi mitatu kwa utovu wa nidhamu na utoro kazini.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo leo kwa vyombo vya habari, kufuatia barua ya kukiri na kuomba radhi kwa makosa kutoka kwa mchezaji huyo na kupitia kwa umakini utetezi pamoja na maelezo yake, kamati ya nidhamu ilikaa na kujadili suala hilo kwa kina.

‘’Baada ya majadiliano hayo, kamati imefikia uamuzi wa kumuondolea adhabu Khalid adhabu ya kusimamishwa kuanzia sasa na kumruhusu kuendelea na majukumu yake kikosini,’’

Huenda mchezaji huyo akaanza kuonekana kuanzia mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaochezwa hapo baadaye kwneye Uwanja wa Airtel mkoani Singida.

Related Articles

Back to top button