Nyumbani

Clement Mzize kufanyiwa upasuaji leo

JOHANNESBURG: MSHAMBULIAJI wa YANGA Clement Mzize, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji leo kufuatia changamoto ya kiafya inayomkabili.

Taarifa za kufanyiwa upasuaji kwake zimewekwa wazi na aliyekuwa mtaalam wa masuala ya misuli na utimamu wa mwili wa Yanga, Seroto Sekhwela maarufu kwa jina la SK Seroto, aliyewapokea nchini Afrika Kusini.

Kupitia ujumbe wake, Sekhwela alionesha mshikamano na upendo kwa nyota huyo akisema:

“Chuma hunoa chuma. Nimempokea mmoja wa wachezaji bora kabisa wa Tanzania pamoja na Dk. Moses Etutu, mchezaji kutoka klabu yangu ya zamani ya Afrika Mashariki, Yanga,

“Sasa ni familia, na leo anaingia kufanyiwa upasuaji. Namtakia nguvu, mikono ya madaktari iwe salama na arejee haraka uwanjani. Tuko pamoja nawe,” amesema.

Mzize alikuwa nje kwa muda mrefu akiuguza jeraha la goti, alipata nafuu na kurejea kwenye mazoezi ambapo alicheza dakika za mwishoni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Far Rabat ya Morocco ugenini na baada yah apo hakuonekana tena ikielezwa kuwa bado hakuwa imara.

Related Articles

Back to top button