Africa

Allan Okello avunja ukimya

DAR ES SALAAM: KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello amesema wameumizwa na kushindwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini bado wana malengo makubwa ya kupigania katika msimu huu.

Okello ametoa kauli hiyo kupitia ujumbe mfupi baada ya Yanga kuhitimisha safari yake katika hatua ya makundi, akieleza kuwa matokeo hayo hayafuti dhamira ya timu kupambana kwenye mashindano yaliyosalia.

“Inasikitisha kutofuzu kwenda hatua inayofuata, lakini bado tuna mengi ya kupigania msimu huu,” ameandika nyota huyo baada ya timu yake kuhitimisha hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Kabylie mwishoni mwa wiki iliyopita Zanzibar.

Kauli ya kiungo huyo inaonesha namna ambavyo wachezaji wa kikosi hicho walivyokuwa na hamasa ya kufanya vizuri kimataifa, licha ya kuishia njiani.

Yanga ilimaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi ya tatu kwenye kundi lake, jambo lililokatisha ndoto za kusonga mbele, lakini sasa nguvu kubwa inaelekezwa kwenye mashindano ya ndani ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho.

Related Articles

Back to top button