Africa
Ndoto ya Yanga kuongoza kundi yayeyuka
NDOTO ya Yanga kuongoza kundi D katika mchuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) imezimika baada kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Al Ahly kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo, Misri.
Hata hivyo Yanga tayari imefuzu hatua ya robo fainali ikiwa na pointi 8 huku Al Ahly ikiwa na pointi 12.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo CR Belouizdad ikicheza kwenye uwanja wa nyumbani wa The 5 July 1962 uliopo Algiers, Algeria imeikanda Medeama kwa mabao 3-0.
CR Belouizdad imefikisha pointi 8 sawa na Yanga huku Medeama ikibaki na pointi 4.
FULLTIME
AL AHLY 1 – 0 YANGA
Hussein Al-Shahat 46′
CR BELOUIZDAD 3 – 0 MEDEAMA
Abdelraouf Benguit 27′
Leonel Wamba 42′
Lamin Jallow 84′