Muziki

Foxxmadeit: Nataka kuipaisha Bongo Fleva Mpaka

BAADA ya kufanikiwa kutayarisha wimbo God Design wa msanii Jux, ambao uliingia kwenye chati za iTunes nchini Nigeria, Foxx anasema sasa anatamani hatua kubwa zaidi.

Mtayarishaji wa muziki anayechipukia kwa kasi, Foxxmadeit, ameweka wazi ndoto yake kubwa ya kuipa Bongo Fleva umaarufu wa kimataifa, akilenga kuipeleka hadi kwenye chati maarufu za muziki duniani, ikiwemo Billboard Hot 100.

“Nataka kutayarisha wimbo utakaoingia kwenye Billboard Hot 100,” amesema kwa kujiamini.

Katika maono yake ya kimataifa, Foxx ameeleza ndoto yake ni kufanya kazi na staa kutoka Afrika Kusini Tyla, lakini pia hakusita kuonyesha imani yake kwa msanii chipukizi wa Tanzania, Abigail Chams.

“Nikimsikiliza Tyla na nikimsikiliza Abigail Chams, nasikia kitu kimoja. Mimi namuona Abby, tumpe muda atafanya mambo makubwa,” amesema Foxx.

Kauli hizi zinaashiria dhamira yake ya dhati kuvuka mipaka ya muziki wa Tanzania na kuifanya Bongo Fleva itambe kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa.

Related Articles

Back to top button