Tiwa Savage: Olamide alikataa milioni 100 nilizompa

ABUJA: MWIMBAJI maarufu, Tiwa Savage amefichua kwamba Olamide alikataa kupokea fedha za Nigeria Naila milioni100 kutokana na sauti yake kusikika katika wimbo wa Tiwa Savage.
Tiwa katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram, alieleza kuwa Olamide, mmiliki wa studio ya YBNL, alikataa pesa hizo baada ya mameneja wake kumlipa baada ya kazi hiyo ya ushirikiano waliyoifanya.
Alibainisha kuwa Olamide hakumtoza fedha zozote huku akieleza sababu ni kutopenda kuona wasanii wa kike wakipitia magumu katika tasnia ya muziki.
Tiwa amefurahishwa na moyo wa rapa huyo aliouonyesha kwake kwa lengo la kusaidia wasanii wa kike.
“Nilikuwa nazungumza na uongozi wake, sikutaka kuzungumza naye moja kwa moja kwa sababu angetaka kufanya hivyo bure. Nilikuwa tayari kulipa na timu yake ilinitoza Naila100milioni lakini Olamide alikataa fedha hizo kupokelewa huku akiwaeleza watu wake wa karibu kuwa mimi ni dada yake na hawezi kuchukua pesa yangu kwa kuwa anataka wasanii wa kike tuwe katika ushindani mzuri kimuziki,” ameeleza.