Kwingineko

Kifo cha Jota: Madrid, Man city waongoza salamu za pole

KLABU Vigogo mbalimbali wa soka duniani wakiongozwa na mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya mabingwa Ulaya na washindi mara nne mfululizo wa ligi ya England Manchester city Pamoja na klabu yake ya zamani ya Wolves ni miongoni mwa klabu zilizotuma salamu za pole kufuatia kifo cha Diogo Jota mshambuliaji wa Liverpool aliyefariki kwa ajali usiku wa kuamkia leo

Taarifa iliyotolewa na Real Madrid imesema Rais wa klabu hiyo na Bodi ya Wakurugenzi wamehuzunishwa sana na kifo cha mchezaji huyo na mdogo wake André Silva, aliyechezea F. C. Penafiel ya ureno. Real Madrid imetoa pole kwa familia na wachezaji wenza katika klabu zao.

Kwa upande wao Manchester City wameeleza kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho kupitia taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya klabu hiyo ikisema kila mtu katika klabu hiyo ameshtuka na kuhuzunishwa na habari mbaya kuhusu kifo cha Diogo Jota. Tunatuma rambirambi zetu za dhati kwa familia yake na marafiki na kila mtu katika Klabu ya Soka ya Liverpool katika wakati huu mgumu.

Klabu yake ya zamani ya Wolves kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika “Tumevunjika moyo. Diogo alipendwa na mashabiki wetu, alipendwa na wachezaji wenzake na alithaminiwa na kila mtu ambaye alifanya kazi naye wakati alipokuwa Wolves. Hakika hatasahaulika. Utakumbukwa kweli, na utakumbukwa kila wakati”

Manchester United kupitia ukurasa wake wa Instagram imewapa pole Liverpoool na mashabiki wake, familia na kila mtu mwenye mapenzi na mchezaji huyo kufuatia Habari ya kifo chake huku wakisema wamevunjika moyo.

Wazee wa darajani Chelsea pia wamesema kila mtu katika klabu hiyo amestushwa na kifo cha Diogo Jota na mdogo wake huku wakieleza kuwa Pamoja na Liverpool, mashabiki na familia ikiwaombea nguvu na Subira katika kipindi hiki kigumu.

Klabu nyingine zilizotoa salamu za pole ni Pamoja na mahasimu wao Everton, Tottenham, Newcastle Unite, West Ham, Nottingham Forest, na Klabu nyongine nyingi za ligi kuu ya England, Laliga na Bundesliga

Related Articles

Back to top button