Mbappe aikodolea macho fainali Copa del Rey

MADRID:KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema mshambuliaji wa klabu hiyo Kylian Mbappe anategemea kuwepo kwenye mchezo wa fainali ya Copa del Rey dhidi ya vinara wa LaLiga na mahasimu wao FC Barcelona jumamosi.
Mbappe ambaye ameukosa mchezo uliopita wa Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao Madrid wakishinda dakika za lala salama bao 1-0 ataukosa pia mchezo wa kesho dhidi ya Getafe baada ya Mfaransa huyo kutolewa kwa tatizo la enka wakati Arsenal ilipoivurumisha nje ya Champions League klabu yake wiki iliyopita.
“Kwenye mchezo wa kesho hatakuwepo, hatakuwa tayari, lakini atafanya mazoezi na wenzake siku mbili hizi na nadhani atakuwepo kwenye El Classico jumamosi. Najua anaumia sana kwa jeraha alilonalo kwa sababu linafanya ashundwe kuisaidia timu namuona akifanya kila awezalo ili acheze jumamosi.”
Mbappe alishangiliwa na mashabiki wa Real Madrid alipoonekana kwenye Screens za Santiago Bernabeu JUmamosi huku ishara hiyo ikiwa Chanya kwa mshambuliaji huyo na sasa Ancelotti anaamini itamsukuma zaidi arejee mapema kwakuwa mashabiki wanamhitaji