Messi: Hatuna uhasimu na Mexico

BUENOS AIRES, Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amepuuzilia mbali madai ya wadau wa soka wa bara la Amerika Kusini kuwa kuna uhasimu unaotokota baina ya timu za taifa za Argentina na Mexico, akisema kuwa uhasimu unaodaiwa na wadau hao wa soka haupo.
Madai ya wadau hao ni baada ya Video za kamera za CCTV katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mechi ya makundi ya Mexico dhidi ya Argentina kwenye Kombe la Dunia la Qatar 2022 kumuonesha Messi akiidharau jezi ya nahodha wa Mexico Andres Guardado, jambo lililozua mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari.
“Wamejiweka kwenye nafasi ya kudai uhasimu na sisi, uhasimu ambao haupo. Hakuna namna unaweza kulinganisha Argentina na Mexico na sijui wanapata wapi nguvu ya kuwa na madai kama hayo” – Messi amesema katika mahojiano na Simplemente Futbol.
Messi amesisitiza kuwa uhusiano wake binafsi na nchi ya Mexico ni chanya na mara zote ameuona upendo wa wazi wa watu wa Mexico kwake na kusema kuwa hajawahi kuwadarau. insisted his relationship with the country remained positive.
Mshindi huyo mara nane wa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka ya Ballon d’Or alilikumbuka goli lake la maamuzi dhidi ya Mexico nchini Qatar, akilitaja kuwa goli lililofufua matumaini ya kikosi chao kutwaa ubingwa likifungwa katika uwanja ambao kwa kiasi kikubwa ulijaa mashabiki wa Mexico.
Messi ameifunga timu ya taifa ya Mexico magoli manne tangu mwaka 2006 huku akiwa hajawahi kupoteza mchezo dhidi yao.




