Mastaa

Chris Brown atuliza ugomvi wa watoto wa Diddy

MWANAMUZIKI kutoka nchini Marekani Christopher Maurice ‘Chris Brown’ aliingilia na kutuliza ugomvi kati ya watoto watatu wa Sean “Diddy” Combs na msanii William Ray ‘Ray J’ katika sherehe ya Halloween iliyofanyika Los Angeles.

Kulingana na chanzo cha habari kilichoiambia Page Six, ugomvi huo ulitokea baada ya Ray J kuonekana akiwa na Amber Rose na meneja wake David Weintraub kwenye maegesho ya magari baada ya sherehe hiyo kumalizika.

Watoto wa Diddy, ambao ni Quincy Brown, 33, Justin Combs, 30, na Christian Combs, 26, walidaiwa kumzingira Ray J wakionyesha kutoridhishwa na kauli alizozitoa hivi karibuni kuhusu baba yao, P Didy ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya mashtaka ya usafirishaji wa binadamu na biashara ya ukahaba.

Ray J alijaribu kupuuza hali hiyo,lakini majibizano yaliongezeka na kuanza kushikana kifua hadi Chris Brown alipokuja kuwaingilia na kumaliza ugomvi huo kabla haujakuwa mkubwa zaidi.

‘’Kuna watu wengi wenye nguvu ambao huenda wakafichuliwa hivi karibuni”amekuwa akisema Ray Jay katika tasnia ya burudani kufuatia mashtaka yanayomkabili P Diddy.

Sean Combs P Didy amekana mashtaka yote dhidi yake na kesi yake inatarajiwa kuanza Mei 5, 2025.

Watoto wa Diddy wamekuwa wakimuunga mkono baba yao, wakipinga taarifa zinazoeleza kuwa mashtaka dhidi ya baba yao ni ya kipuuzi.

Related Articles

Back to top button