Africa

Yanga yaondoka na pointi 1 Ghana

KLABU ya Yanga imetoka sare ya bao 1-1 na Medeama ya Ghana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kwenye uwanja wa Baba Yara uliopo mji wa Kumasi, Ghana.

Mchezo mwingine wa kundi D umezikutanisha Al Ahly iliyoikaribisha CR Belouizdad ambapo zimetoka suluhu.

Yanga itarudiana na Medeama Desemba 20 Dar es Salaam huku CR Belouizdad ikiikaribisha Al Ahly huko Algeria.

Msimamo wa kundi D ni kama ifuatavyo:

# TIMU P W D L F A GD PTS
1 Al Ahly 3 1 2 0 4 1 3 5
2 Medeama SC 3 1 1 1 3 5 -2 4
3 CR Belouizdad 3 1 1 1 4 2 2 4
4 Yanga 3 0 2 1 2 5 -3 2

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button