Nyumbani

Yanga yaachana na Yacouba Songne

KLABU ya Yanga leo imetangaza kuachana na mshambuliaji wake Yacouba Songne.

Hatua hiyo inafuatia sakata la muda mrefu kuhusu hatma ya mchezaji huyo wa kimataifa mzaliwa wa Bobo-Dioulasso, Burkina Faso.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Yanga imeandika: “π—”π—¦π—”π—‘π—§π—˜ Yacouba SongneπŸ™πŸ½.Tunakutakia kila heri na mafanikio.”

Awali Yacouba kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram amewashukuru mashabiki na viongozi wa Yanga kwa ushirikiano wao.

“Ulikuwa wakati mzuri tangu tulipokuwa pamoja mpaka sasa asanteni kwa upendo wenu kwangu na ushirikiano wenu kuanzia kwa wachezaji hadi uongozi wote wa yanga na mashabiki daima nitawakumbuka hadi wakati mwingine wananchi asante sana na kwaherini, nawapenda,” amesema Yacouba.

Related Articles

Back to top button