Nyumbani

Yanga uso kwa uso na Red Arrows siku ya Mwananchi

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imetangaza itacheza mechi ya kirafiki na Mabingwa wa Zambia na michuano ya kombe la Kagame, Red Arrows katika kilele cha siku ya Wananchi itakayofanyika Agosti 4, mwaka huu, Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar Es Salaam

Akizungumza na waandishi wa habari za michezo makao makuu wa klabu hiyo katika uzinduzi wa siku ya Wananchi, Afisa uhamasishaji wa Yanga Haji Manara ameweka wazi kuwa shamrashamra zinaanza leo kwa kupokea kikosi cha timu hiyo kikitokea Afrika Kusini wakiwa mabingwa wa kombe la Toyota.

Amesema kikosi hicho kinarejea na kuingia kambini kwa ajili ya kuajiandaa na mchezo huo wa wiki ya wananchi ambayo watacheza dhidi ya Mabingwa hao wa Zambia kwa ajili ya kujiweka vizuri kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25.

“Champion wa Kagame Cup msimu huu, Red Arrows kutoka Zambia ndio timu tutakayocheza nayo siku ya Agosti 4, pale uwanja wa Benjamin Mkapa, wametuambia watakuja na Ndege yao ya Jeshi,” Msemaji wa Yanga Sc, Haji Manara.

Amesema mechi itakuwa nzuri sana na waratibu wamefanya kazi kubwa na kuwahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa atafanya utambulisho wa wachezaji wa kimataifa siku ya Wananchi.

Ameongeza kuwa kikosi hicho kinatua nchini saa 9 usiku na wachezaji wenda kambini huku kombe likibaki kwa mashabiki walihudhuria uwanja wa ndege na kufanya parede la kombe hilo hadi makao makuu ya klabu hiyo kupeleka kombe hilo.

Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kununua tiketi mapema kwa ajili ya kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuwaonyesha watu Yanga ni mabingwa wa mara nyingi Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button