Yanga kuifuata Al Hilal Okt 14


TIMU ya soka ya Yanga, inatarajia kwenda Sudan Oktoba 14 kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal.
Katika mchezo wa kwanza Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 na Al Hilal kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Ili kusonga mbele inatakiwa kushinda au kutoka sare kuanzia mabao 2-2 na kuendelea katika mchezo huo wa marudiano.
Akizungumza na Spotileo, Meneja wa timu hiyo Walter Harrison amesema:“Ni mchezo mgumu ambao tunahitaji matokeo ya ushindi ili kwenda hatua inayofuata,” amesema Harrison.

Amesema taratibu zote za safari hiyo zinakwenda vizuri sambamba na maandalizi ya timu kwa ajili ya mchezo dhidi ya Al Hilal.
“Tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda na kusonga mbele hatua ya makundi,”amesema Harrison.