
MECHI tatu za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) zinapigwa leo kwenye viwanja tofauti.
Miamba ya Afrika, Misri itakuwa ugenini kuivaa Guinea ukiwa mchezo wa kundi D kwenye uwanja wa Grand Marrakech uliopo Morocco.
Sudan Kusini ipo uwanjani hivi sasa kuikabili Gambia kwenye uwanja wa Suez Canal uliopo Ismailia, Misri katika mchezo wa kundi G ambapo ni dakika ya 23 na timu hizo zipo sare ya bao 1-1.
Katika kipute kingine Guinea-Bissau itakuwa nyumbani kuivaa Sao Tome na Principe kwenye uwanja wa September 24 katika jiji la Bissau.