Ligi KuuNyumbani

Yanga kuendeleza ubabe leo?

BAADA ya kufikisha michezo 49 ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila kufungwa vinara wa ligi hiyo Yanga leo inashuka dimbani mkoani Mbeya kuwavaa wenyeji Ihefu.

Mchezo pekee wa ligi leo utapigwa uwanja wa Highland Estates uliopo eneo la Ubaruku, Mbarali.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na Pointi 32 baada ya michezo 12 wakati Ihefu ipo nafasi ya 16 mwisho wa msimamo ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 13.

Sehemu ya wachezaji wa Ihefu wakifanya mazoezi.

Michezo miwili ya ligi hiyo imepigwa Novemba 28 ambapo KMC na Tanzania Prisons zimetoka suluhu katika uwanja wa Uhuru wakati Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Related Articles

Back to top button