LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kufanyika Dar es Salaam na Lindi.
Katika mchezo wa Dar es Salaam Azam itaikaribisha KMC kwenye uwanja wake wa Azam Complex uliopo Chamazi.
Azam inashika nafasi katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 baada ya michezo 10 huku KMC ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 11.
Katika kipindi cha miaka sita iliyopita Azam imeifunga KMC mara tano, zimetoka sare mara mbili na KMC imeifunga Azam mara tatu.
Katika mchezo mwingine Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 mwisho wa msimamo wa ligi ikiwa na pointi tano baada ya michezo 11 wakati Namungo inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 14 baada michezo 12.
Katika kipindi cha miaka sita iliyopita Namungo imeifunga Mtibwa Sugar mara nne, zimetoka sare tatu wakati Mtibwa Sugar imeifunga Namungo mara moja.