Fadlu: Bahati yao! nilitaka kuwamaliza mapema

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amebainisha kuwa walistahili kupata idadi kubwa ya mabao kipindi cha kwanza kabla ya kwenda mapumziko kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc.
Amesema walistahili kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao matatu lakini hawakuweza kutumia vizuri nafasi walizopata katika mchezo huo uliopigwa Septemba 26, Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
Fadlu amesema walikuwa wanahitaji kupata pointi tatu muhimu na ilikuwa hivyo kutokana na mpango kazi uliopangwa, wameibuka na ushindi jambo ambalo ni furaha kwao.
“Tumefurahi kupata ushindi kwenye mchezo wetu muhimu na ilikuwa hivyo kikubwa ni kwamba kila mchezaji alikuwa anatambua kwamba tunahitaji pointi tatu na walicheza kwa kujituma mwanzo mwisho kwa ajili ya kupata matokeo mazuri uwanjani wanastahili pongezi wachezaji wetu,” amesema kocha huyo.
Amewapongeza wachezaji na wasaidizi wake wa benchi la ufundi kwa kazi nzuri waliyoifanya kuiwezesha timu kupata ushindi dhidi ya Azam FC.
Kocha huyo amesema kazi bado inaendelea kwani wana mchezo mwingine dhidi ya Dodoma Jiji na wameshafanya maandalizi kwa ajili ya kuwakabili wapinzani ili kupata pointi tatu muhimu ugenini