Africa

Vigogo watishia kuibomoa Simba

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa klabu ya Simba, umeweka wazi na kusema kuwa hauna mpango wa kuachana na kocha wao, Fadlu Davids anayetajwa kutakiwa na klabu mbalimbali ikiwemo As Far Rabati ya Morocco.

Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vilieleza kuwa Fadlu amekuwa akitajwa na klabu ya As Far Rabati ikiangalia uwezekano wa kupata huduma yake.

Akizungumza na Spotileo, Meneja wa idara ya habari na mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally amesema Fadlu ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kulingana na makubaliano waliokubaliana mwanzoni mwa msimu huu.

“Kocha Fadlu tunae na tunatamba naye, sisi sio wale wanakimbiwa na makocha, ataendelea kusalia kukinoa kikosi cha Simba, kutufikisha katika malengo yetu,” amesema.

Ahmed amesema mashabiki wamekuwa wakibeba ujumbe ambao unamuheshimisha kocha huyo ambaye anaipeleka Simba kule wanapotarajia.

“Ukiangalia mchezo wetu wa leo (jana) na Tanzania Prisons, mashabiki wamebeba jumbe mbili moja kumkubalia kocha wetu, ujumbe wa Ladack Chasambi kwa kumpa moyo, hii inaonyesha jinsi gani wanachama wetu wanaungana na viongozi,” amesema.

Related Articles

Back to top button