Filamu

Van Damme akana kuhusika na biashara haramu ya binadamu

UFARANSA: MCHEZA filamu mashuhuri Jean-Claude Van Damme amekana madai ya biashara haramu, anayotuhumiwa nayo huku akiyataja kuwa ya kipuuzi.

Muigizaji huyo amewaita waliomshitaki hawana misingi n ani wapuuzi kwa kuwa madai hay oni ya kizushi kwake hawezi kujihusisha na biashara haramu za binadamu.

Wakala wa muigizaji huyo, Patrick Goavec, aliiambia PEOPLE: “Tumefahamu makala zinazodai kuwa na uhusiano wa kimapenzi huko Cannes unaomhusisha Jean-Claude Van Damme. Ukweli ulioripotiwa ni wa kuchukiza na haupo kabisa. Van Damme hataki kutoa maoni au kuchochea uvumi huu, ambao ni wa kipuuzi kwani hauna msingi,”.

Malalamiko hayo yanadai kuwa Jean-Claude Van Damme mwenye miaka 64, alijihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanawake ambao walikuwa wakisafirishwa na mtandao wa uhalifu unaoongozwa na Morel Bolea, mfanyabiashara wa Kiromania na mmiliki wa wakala wa wanamitindo mbalimbali.

Kisa hicho kinaripotiwa kutokea katika hafla iliyoandaliwa na muigizaji huyo Van Damme huko Cannes. Mmoja wa mashahidi hao anayedai kuona tukio hilo likiendelea, alitoa ushahidi kwa waendesha mashitaka, na kusababisha DIICOT kuanzisha uchunguzi wa makosa ya jinai.

Jean-Claude Van Damme anajulikana kwa kuonekana katika waigizaji kama vile ‘Bloodsport’, ‘Kickboxer’ na ‘Timecop’ na mara ya mwisho alionekana katika filamu ya Ufaransa, ‘The Gardener’, iliyotoka Januari 2025.

Related Articles

Back to top button