EPL

Usajili bora zaidi EPL 2023/2024

KUFUNGULIWA kwa dirisha lolote la usajili mara nyingi huja kwa harakati zenye mashaka, lakini pia kunatoa msisimko kama lengo la timu kuimarisha kikosi kukabiliana na changamoto zinazoikabili.

Baadhi ya wachezaji wapya huzoea mazingira mapya papo hapo majira ya kiangazi na dirisha dogo Januari, ambapo wengine huhitaji muda zaidi kupata matokeo bora.

Ufuatao ni usajili bora zaidi wa wachezaji wa klabu kadhaa Ligi Kuu England(EPL) msimu wa 2023/2024.

1.Declan Rice (Arsenal)
Rice amekuja kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa kikosi cha Mikel Arteta.

2.Cole Palmer (Chelsea)
Palmer alimshinda kila mchezaji Stamford Bridge hadi kuwa mchezaji bora wa msimu kijana wa EPL.

3. Alexis Mac Allister (Liverpool)
Alithibitisha ni hatari akicheza namba 6 kuzipa pengo lililoachwa na Jordan Henderson na Fabinho.

4.Moussa Diaby (Aston Villa)
Diaby amechangia kwa kiasi kikubwa idadi ya mabao tangu alipojiunga na Villa.

5.Kai Havertz (Arsenal)
Ingawa hakuanza vema msimu, baadaye kiwango cha Havertz kilistaabisha, akitokea kuwa hatari kwa mipira ya juu wakati pia akiiunganisha timu.

6.Micky van de Ven (Tottenham Hotspur)
Kasi yake na kujiamini kulimfanya kuwa kivutio na mchezaji wa kuogopewa.

7.Mohammed Kudus (West Ham United)
Kudus ni mwepesi, mwenye nguvu na kipaji cha kiufundi, hivyo kuwa aina halisi ya mchezaji West Ham iliyomhitaji.

8.Ross Barkley (Luton Town)

Baadhi walimdharau, lakini Barkley aliwanyamazisha wenye chuki ingawa timu yake imeshuka daraja.

9. Joao Pedro (Brighton & Hove Albion)

Kwa haraka Pedro aliibuka shujaa na kumfunika mchezaji mwenzake nyota wa Brighton, Evan Ferguson.

10.Adam Wharton (Crystal Palace)

Ubora wake wa kutoa pasi na kutafuta nafasi uwanjani umesababisha aitwe kwenye kikosi cha awali cha timu ya taifa ya England.

Picha/Habari: 90min.com

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button