Umeshapata mwenza? Sasa ushindwe mwenyewe
DAR ES SALAAM ; Shindano la Hello Mr Right! msimu wa sita limezinduliwa rasmi vijana wakihimizwa kutumia nafasi ya kufuatilia kujifunza namna ya kupata wenza sahihi wa maisha yao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Godfrey Lugalabam ‘Gara B’ amesema kuwa msimu huu umekuja kitofauti kwa kuongeza watu wapya wa kutoa mafunzo huku Kaulimbiu yao ikiwa ni ‘Usione so’
“Lengo ni kuwakutanisha watu wanaotafuta wenza na kuwaunganisha pamoja waweze kutimiza malengo yao ya kujenga familia ya pamoja.”amesema Gala B
Kwa upande wake mtangazaji wa kipindi cha Hello! Mr Right Aliya Mohammed amesema kuwa Shindano hilo huchukua wadada 12 ambapo watatafuta wenza wao ambao kwao ni Mr Right! mmoja.
“Watu wasichukulie Hello! Mr Right kama Shindano la kiuni hapana Shindano hili lina maadili yote na ndio sababu tunawakutanisha kisha kuwapa ushirikiano katika kutimiza kiapo cha ndoa.”amesema
Swalehe Nasoro ‘Dokta Kumbuka’ amesema kuwa atakuwepo kwaajili ya kuwapa somo washiriki katika kuchagua mtu sahihi katika maisha yake.
“Wadada wengi wanajidanganya kuwa mwanaume sahihi ni yule mwenye muonekano mzuri au mwenye pesa unaweza mpata mtu sahihi hasiwe na pesa wala muonekano fatilia utataona sifa za mwanaume sahihi.
Naye Meneja Masoko wa Startimes David Malisa amesema kuwa msimu wa sita wa Mr Right niwakitofauti ukizingatia ndio Shindano la kwanza la kiswahili lenye mazuri mengi.
“Usione so kutazama msimu huo usipange kukosa Hello! Mr Right tumepata wadada zaidi ya 450 na wanaume 800 wakitaka kukutanishwa na wapenzi sahihi kupitia Shindano hilo.”amesema Malisa
Meneja Biashara wa St Bongo Magreth amesema kuwa Makampuni na watu mbalimbali wanaweza kujitokeza kuamini shindano hilo.
Raul Khan Meneja vipindi kutoka St bongo amesema kipindi kitaruka kila jumamosi, jumapili, Jumanne , Jumatano na kuwahimiza watu wasikose kwani kutakuwa na zawadi na surprise za kutosha.