Nyumbani

Tundaman: Sina Ubaya na Uongozi wa Simba

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa kizazi kipya na shabiki wa Simba, Khalid Ramadhani (Tundaman), amesema hana shida na uongozi wa Simba,huku akisema ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ndio sababu ya kutoimba siku ya kilele cha Simba Day.
 
Amesema alipokea ujumbe kutoka kwa mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba , Mohammed Dewji akimtaka awe sehemu ya wasanii siku ya jana uwanja wa Benjamin Mkapa , jijini.
 
Kutokuwepo kwa Tundaman ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaoishabikia Simba na mara zote amekuwa sehemu ya kuwapa burudani, kuliibua maswali na kwenda mbali zaidi kuwa huenda msanii huyo amenyimwa shoo na kuamua kuhamia Yanga.
 
“Kwanza niwaombe msamaha viongozi wangu wa Simba, majukumu niliyokuwa nayo nje ya uwezo wangu nimeshindwa kuwa sehemu ya wasanii ambao waliimba katika tamasha.
 
Nilikuwa katika ziara Mvomero na nimerudi tayari Shoo imeisha na kushuhudia timu yangu ya Simba ikicheza. Mo Dewji aliniambia niimbe siku ya kilele lakini nimeshindwa. Mimi bado nitabaki kuwa Simba, hata waniue Simba sihami,” amesema msanii huyo.
 
Ameongeza kuwa ameiona timu yao ya msimu ujao na kujipanga kwa ajili ya kuendelea kushusha mistari juu ya kuiimbia timu yake hiyo ya Simba .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button