Wenye ulemavu kuzingatiwa kwenye Miundombinu viwanjani

DODOMA: SERIKALI imesema itahakikisha kunakuwa na umakini katika usimamizi wa viwanja vinavyojengwa nchini na kukarabatiwa miundombinu ya watu wenye mahitaji maalum na kuweza kutumika na makundi yote ikiwemo wenye ulemavu.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni Jumatano, Januari 29, na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo,Hamis Mwinjuma wakati akijibu swali la Mbunge Mwatatu Mbarak Khamis aliyetaka kujua Serikali imejipangaje kuhakikisha kuwa viwanja vya michezo kwa watu wenye ulemavu vinaendelea kuwepo na vinaimarishwa.
Mwinjuma amesema uzingativu huo unatolewa kwa wadau na taasisi zote zinazomiliki na kuendesha miundombinu ya michezo wanaweka maeeneo maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu kuweza kushiriki wakati wa matukio ya kimichezo.
“Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam ambao umezingatia hilo pamoka na uwanja wa unaojengwa jijini Arusha, Samia Suluhu Stadium,Wizara imeendelea kutoa vifaa vya michezo kwa watu wenye mahitaji maalumu hasa katika ngazi ya timu za Taifa ndani ya kundi hili maalum kuwawezesha kutumia viwanja vilivyopo,” amesema.