Bundesliga

Tullberg aumaliza mwendo Dortmund

HEIDENHEM: KOCHA wa muda wa Borussia Dortmund Mike Tullberg amesema atarejea kwa furaha katika timu ya vijana wa chini ya miaka 19 ya klabu hiyo baada ya mchezo wa Bundesliga wa wikiendi hii dhidi ya Heidenheim kesho Jumamosi ikihitimisha kile alichokiita fainali zake 3.

Kocha Tullberg aliichukua Dortmund kama mwokozi baada ya kufukuzwa kwa kocha Nuri Sahin aliyekuwa anazamisha jahazi la vigogo hao wa Bundesliga kufuatia vipigo vinne mfululizo kwenye mashindano yote.

Kocha huyo wa timu ya vijana aliisaidia Dortmund kwenye sare ya 2-2 na Werder Bremen kisha kupata ushindi wa kwanza wa 3-1 mbele ya Shakhtar Donetsk ushindi ambao umewapa nafasi ya kucheza dhidi ya Sporting kwenye playoff ya kuisaka 16 bora.

Tullberg amewaambia waandishi wa habari kuwa kupata nafasi ya kuongoza timu hiyo ya wakubwa ni heshima kwake na haitambadilisha kimtazamo wala kumuongezea kiburi.

“Mimi ni yule yule, mpira ni mpira na watu ni watu ni rahisi kubadilisha mchezo uwanjani lakini si mchezaji, michezo hii mitatu nimeiendea kama fainali nimemaliza mbili na ya mwisho ni kesho. Nimemaliza ninarudi kwenye timu ya vijana, mara zote haijawa kwa ajili yangu ni kwa ajili ya klqbu” – Amesema

Dortmund wameshinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo yao 8 iliyopita wakidondoka mpaka nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Bundesliga wakihatarisha nafasi yao kwenye ligi ya mabingwa msimu ujao.

Jana vigogo hao walimtangaza Kocha wa zamani wa Bayern Munich Niko Kovac kama kocha wao mpya

Related Articles

Back to top button