Africa

Timu za Afrika zamkuna Motsepe kwenye Kombe la Dunia

JOHANNESBURG: RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe amesema anajivunia viwango vya timu 10 za Afrika zilizopambana katika Kombe la Dunia 2026 lililomalizika Jumapili iliyopita.

Motsepe ameyasema hayo leo Jumatano alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kufungua mpango wao wa kushirikiana kwa ukaribu zaidi na makocha kuhakikisha msimu ujao wanakuwa bora zaidi.

Katika michuano hiyo ambayo bingwa iliibuka Uhispania kwa kuifunga Argentina bao 1-0,
Afrika iliwakilishwa na timu 10; Algeria, Cape Verde, Côte d’Ivoire, DR Congo, Misri, Ghana, Morocco, Senegal, Afrika Kusini na Tunisia.

Na tisa kati ya hizo, zilifuzu kutoka makundi hadi hatua ya 32 bora, sawa na 90%.

Hiyo imeifanya Afrika na CAF kuweka rekodi ya kiwango cha juu zaidi cha asilimia katika historia ya mashindano hayo.

Mafanikio hayo yalifuatiwa na timu za UEFA pekee, ambayo ilikuwa na asilimia 40 ya timu zake za taifa zilizofuzu hatua ya 32 bora.

Kipekee, Motsepe alizisifia Misri na Morocco zilizofika hatua ya 16 bora ingawa Morocco ilisonga mpaka robo fainali kabla ya kusukumwa nje na Ufaransa kwa mabao 2-0.

“Lakini pia tumebainisha maeneo mahususi ambapo kuna nafasi za kuboresha, na nina imani kuwa makocha, timu za ufundi na wachezaji watafanyia kazi maboresho hayo yanayohitajika.

“CAF itaandaa mkutano na kuwaalika makocha wa timu za taifa, timu za ufundi, wachezaji wa zamani wa timu za taifa za Afrika pamoja na wataalamu wengine wa soka na wadau ili kutathmini viwango vya timu za Afrika katika Kombe la Dunia 2026, kwa lengo la kutoa mapendekezo yatakayohakikisha kuwa timu za Afrika zinafanya vizuri zaidi katika Kombe la Dunia 2030,” alisema Motsepe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button