Nyumbani

Kufuzu AFCON Stars kumenyana na Guinea Bissau

DAR ES SALAAM:TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itaanza kampeni ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 kwa kucheza dhidi ya Guinea-Bissau, Septemba 25, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10 jioni, huku Taifa Stars ikijiandaa kuendelea na ratiba ya mechi za kufuzu kwa michuano hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam Leo Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Clifford Ndimbo amesema baada ya mchezo huo, timu inatarajiwa kuondoka Septemba 26 kuelekea Casablanca, Morocco, kwa ajili ya mchezo wa pili dhidi ya Madagascar, utakaochezwa Septemba 29.

Madagascar itatumia Morocco kama uwanja wake wa nyumbani.

Aidha, Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Ghana, Oktoba 4, katika jiji la Casablanca, Morocco.

“Ratiba hiyo ni sehemu ya maandalizi na majukumu ya timu za taifa katika kipindi hiki cha kalenda ya kimataifa ya soka,”amesema.

Related Articles

Back to top button