Nyavu
Timu nne zatinga nusu fainali wavu taifa
DAR ES SALAAM: LIGI ya Wavu taifa ikio hatua ya mtoano ambapo timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali.
Timu zilizotinga ni Tanzania Prisons, Jeshi Stars, High Voltage na Bandari ambazo zina kazi ya kupambania fainali.
Timu hizo zimetinga hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika michezo yao yar obo fainali.
Tanzania Prisons iliifunga JKT kwa seti 3-1, huku Jeshi Stars ikiibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Milambo VC.
High Voltage nayo ilipata ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Nyika VC, wakati Bandari ikiifunga KIUT kwa seti 3-0.




