Nyavu

Bandari, JKT mambo safi wavu

DAR ES SALAAM: TIMU za Bandari, JKT na Jeshi Stars zimeendelea kufanya vyema katika kampeni zao, Ligi ya Taifa ya Wavu baada ya kuibuka na ushindi katika michezo iliyochezwa jana.

Bandari ilionesha ubora wake kwa kuichapa Moro Warriors kwa seti 3-0 katika mchezo uliotawaliwa na mabingwa hao kuanzia mwanzo hadi mwisho.

JKT nayo ilipata ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Nyika VC baada ya mchezo wa ushindani ulioshuhudia Nyika ikijitahidi kurejea lakini ikashindwa kuzuia kasi ya wapinzani wao.

Kwa upande mwingine, Jeshi Stars ilitumia vyema nafasi zake na kuibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Police Tanzania VC, matokeo yaliyoifanya kuanza ligi kwa pointi muhimu.

Michuano hiyo inaendelea leo ambapo Milambo itavaana na Moro Warriors, Chui itachuana na Nyika VC, huku TPDC ikitarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Police Tanzania VC katika mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Related Articles

Back to top button