Ligi Kuu

Tabora United kuhamia CCM Kirumba kwa michezo ya nyumbani

TABORA: UONGOZI wa Tabora United umetangaza rasmi kuwa michezo yao yote ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, baada ya Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kufungiwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Christina Mwagala, ambaye amesema kuwa timu itaanza kutumia uwanja huo kuanzia mchezo dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Ijumaa, Machi 7.

Aidha, Christina amewahakikishia mashabiki wa timu kuwa juhudi zinaendelea kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Tabora pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha uwanja wao wa nyumbani unakarabatiwa na kuwa tayari kwa matumizi katika siku zijazo.

Kwa sasa, CCM Kirumba utakuwa kimbilio la Tabora United katika harakati zao za kusalia kwenye ligi huku wakitarajia kupata sapoti kutoka kwa mashabiki wa Mwanza na mikoa jirani.

Related Articles

Back to top button