Stevo Simple Boy apigwa risasi mrembo amuokoa

NAIROBI: VIDEO ya msanii wa Kenya, Stevo Simple Boy umeonekana kupata watazamaji wengi kutokana na video ya wimbo huo ikimuonyesha msanii akivaa uhusika wa jambazi mwenye huruma kwa wanawake warembo.
Wimbo huo unaitwa ‘Vile Inafaa’ ameuachia mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii lakini imekuwa na maoni mengi huku wengi wakimsifia kwa ubunifu alioufanya katika video hiyo na namna alivyopangilia matukio ya video hiyo.
Katika video hiyo, Stevo na kundi la vijana wa kazi wenzake walioziba nyuso zao wakivamia benki kwa lengo la kufanya uharifu lakini Steve anavutiwa na mwanamke mrembo anayemuona pembeni akiwa anafanya wizi huo.
Video inaendelea kuonyesha kwamba wakati wanatoka katika benki hiyo Stevo Simple Boy anapigwa risasi na mwanamke huyo anamwokoa na kumpeleka hospitali.
Mrembo huyo anakuwa muuguzi baada ya kupona wanakutana kwa mazungumzo na kuanzisha uhusiano baada ya kuharikana kwenye chakula cha jioni.