Slot ni shabiki wa Postecoglou

LONDON: Meneja wa vinara wa ligi kuu ya England Liverpool FC Arne Slot amesema yeye ni shabiki mkubwa wa staili ya uchezaji ya meneja wa Tottenham Hotspur Ange Postecoglou na anatamani Spurs washinde kombe ila si la Carabao.
Vinara hao watawavaa na Spurs katika ligi kuu Jumapili hii kabla ya kuvaana tena kwenye nusu fainali ya kombe la Carabao mapema mwezi Januari 2025
“Mimi ni shabiki wa Ange napenda aina yake ya uchezaji, natumai natumai na natumai ashinde kombe japo sio hili la Carabao. Nawashabikia kwenye Europa League pia. Watu wanapenda kuzungumza mataji mataji mataji na taji la Europa league ni muhimu” amesema
“Kwangu aina yake ya mchezo ni ya muhimu sana, na kama ataweza kuongeza kitu, utakuwa mpira mzuri sana kwa ujumla ili sasa watu waache kumsema anacheza soka la kushambulia sana” – ameongeza Slot
Spurs wanafukuzia taji lao la kwanza tangu 2008 na tayari wapo nusu fainali ya Carabao Cup baada ya kuichapa United 4-3 na sasa watawakaribisha Liverpool kabla ya kwenda kumaliza utata Anfield.