Kwingineko

“Sina mpango wa kuondoka City” – Ederson

PHILADELPHIA, Mlinda lango wa Manchester City, Ederson Morales amesema taarifa zozote zinazohusu kuondoka kwake katika klabu hiyo katika misimu ya hivi karibuni ni habari za uongo wakati huu anapoingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake.

Mbrazil huyo anahusishwa pakubwa na kuhamia Katika ligi kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League) akitaja kuwa amepokea “ofa zisizo za kawaida” mwezi Oktoba kutoka katika ligi hiyo, lakini amewaambia waandishi wa habari kuwa moyo wake upo Man City.

“Kuna habari nyingi sana za uongo zinazunguka jina langu. Nataka niwaambie kuwa Kichwa changu kiko hapa, kinabaki na City. Timu hii Inanipa kila kitu kurejea Ligi Kuu tena na kujaribu kushinda Ligi ya Mabingwa pia. Akili yangu inabaki katika klabu hii.” amesema Ederson

Awali Kocha wake Pep Guardiola alisema hajui lolote kuhusu mkataba wa Ederson. Ikiwa Man City haitamuongezea mkataba, Kipa huyo ataondoka kama mchezaji huru mwaka ujao.

Guardiola alisema: “Ninachoweza kusema, ninafurahishwa sana na kile ninachokiona kwenye mazoezi na ninafurahi kwamba Eddie bado yuko nasi”

“Hatuwezi kuvuta picha tungefanya nini kwenye miaka 10 hii ya mafanikio bila yeye. Mchango wake umekuwa mkubwa katika nyanja nyingi sana na nimefurahishwa sana.”

Ederson amekuwa namba moja wa City tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Benfica mwaka 2017. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ameshinda mataji mbalimbali yakiwemo sita ya Ligi Kuu ya England na moja la Ligi ya Mabingwa huku pia akiwa ametwaa tuzo ya Golden Glove mara tatu kwa kuwa na clean sheets nyingi.

Related Articles

Back to top button