Mapinduzi CupNyumbani
Ukame magoli Amaan kumalizika leo?

BAADA ya michezo mitatu kufanyika uwanja wa New Amaan Complex ikiwemo miwili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi bila kushuhudiwa goli, michezo ya kombe hilo inaendelea leo kwa mechi mbili.
Katika mchezo wa kwanza leo KVZ itaivaa Jamhuri huku mechi ya pili ikizikutanisha JKU na Singida Fountain Gate.
Mchezo wa ufunguzi uwanja wa New Amaan Complex ulishuhudia Zanzibar Heroes ikitoa suluhu na Kilimanjaro Stars, huku mechi za Azam dhidi ya Mlandege na Chipukizi dhidi ya Vital’O pia zikiwa suluhu