Nyumbani

Simba yaruka na wazee wa Yanga

DAR ES SALAAM:MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema msimu huu hawaonei mtu aibu na wameamua kufanya ubaya ubwela katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kauli hiyo ya Ahmed imekuja baada ya wazee wa Yanga jana kuita kikao na kudai kuwa Simba inatumika kuharibu mipango ya Yanga, ikiwemo kucheza mechi yao.

Baada ya kauli ya wazee hao, Ahmed amesema watani wao wanapoona dalili ya kuzidiwa wanatumia wazee wao kutishia watu, lakini mwaka huu hata waende wapi, Mnyama ataendelea kufanya ubaya ubwela katika kila eneo.

“Hatutaacha kwa vitisho kisa wazee, huu mpira wa miguu tutahangaika nao. Waache wazungumze, tunaendelea kupeleka moto, mwaka huu hatumuonei mtu aibu, tunataka heshima yetu mjini.

“Tumewashtukia, hiyo ni mipango yao, wakiona mambo magumu wanatumia wazee hivyo tutaruka nao. Simba imedhamiria kufanya kweli msimu huu kutafuta ubingwa wa Ligi Kuu,” amesema.

Ahmed ameongozana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Simba, Zubeda Hassan, ambapo wamesafiri kwenda Qatar kwa ajili ya droo ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika kesho nchini humo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button