Ligi KuuNyumbani

Nitahakikisha timu inapata matokeo mazuri-Medo

KOCHA Mpya wa Dodoma Jiji, Melis Medo ameahidi kuirudisha timu hiyo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada kuridhishwa na viwango vya wachezaji waliopo.

Akizungumza na Spotileo Medo amesema kitu cha msingi ni ushirikiano kutoka kwa uongozi pamoja na wadau wa soka wa mkoa wa Dodoma ili kuhakikisha timu yao inautumia vizuri uwanja wa Jamhuri kushinda kila mchezo.

Ameushukuru uongozi wa timu hiyo kwa kutambua uwezo wake na kumpa jukumu hilo la kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri kwenye ligi na mashindano mengine watakayoshiriki.

“Kwa kutumia ujuzi wangu katika kufundisha soka na ubora wa wachezaji niliowakuta kwenye timu naamini tutatimiza malengo,” amesema Medo.

Oktoba 10, 2022 uongozi wa Dodoma Jiji ulimfuta kazi kocha Masoud Djuma Irambona raia wa Burundi kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Medo aliwahi kuzifundisha timu kadhaa nchini zikiwemo Coastal Union na Gwambina.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button