Nyumbani
Ndumbaro ajiuzulu uenyekiti
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro amejiuzulu uenyekiti wa Kamati wa Rufani ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF katika barua yake kwa Rais wa shirikisho hilo, Dk Waziri amesema kutokana na wadhifa wake mpya inamlazimu kujiuzulu wadhifa huo.
TFF imesema: “Amelazimika kujiuzulu nafasi hiyo ili atekeleze majukumu aliyopewa kwa haki na kuepusha mgongano wa maslahi.”
Dk Ndumbaro aliteuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo Agosti 30, 2023.