Ligi KuuNyumbani

Denis Kitambi ‘bye bye’ Namungo

KLABU ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Namungo imetangaza kuchana na kocha wake Dennis Kitambi.

Taarifa ya Namungo kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii imesema: “Uongozi wa Namungo Fc unapenda kumshukuru Kocha Denis Kitambi kwa muda wote aliotumikia timu kwa ushirikiano mkubwa ndani ya timu yetu.”

Kitambi alijiunga na Namungo mwisho wa mwaka 2022.

Namungo inashika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 13.

Related Articles

Back to top button