Ligi KuuNyumbani

Mtibwa, Polisi mtihani Ligi Kuu leo

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo minane kupigwa viwanja tofauti.

Yanga ambayo tayari imetwaa ubingwa ipo mkoani Mbeya ikiwa mgeni wa Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine.

Miamba ya soka Simba ni mwenyeji wa Polisi Tanzania yenye pointi 25 na inahitaji ushindi kujinasua kutoka kwenye janga la kushuka daraja.

Mechi hiyo itapigwa uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Patashika nyingine itakuwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Azam inayowania nafasi za nne za juu katika msimamo wa liigi itakapoikabili Coastal Union.

Ihefu ambayo mwanzo wa ligi ilikuwa hoi lakini baadaye ikarejesha makali itakuwa mwenyeji wa Geita Gold kwenye uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali, Mbeya.

Huko Turiani mkoani Morogoro kuna #sukariderby ambapo Mtibwa Sugar iliyopo katika hatari ya kushuka daraja itaikaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Manungu.

Ruvu Shooting ambayo tayari imeshuka daraja itakuwa mgeni wa Singida Big Stars ambayo inawania nafasi nne za juu.

Maafande wa Tanzania Prisons watakuwa uwanja wao wa nyumbani wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga kuikaribisha KMC ambayo nayo ikipoteza mchezo pia itakuwa hatarini kushuka daraja.

Katika mchezo mwingine Dodoma Jiji imesafiri hadi mkoani Lindi ikiwa mgeni wa Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa.

Related Articles

Back to top button