Tetesi

‘Thank You’ za Yanga kuanza Jumatatu, panga kupita kwa hawa

DAR ES SALAAM: HATMA ya mastaa watatu wa kigeni ndani ya kikosi cha wababe wa soka la Tanzania Young Africans kujulikana Julai Mosi mwaka huu wakati uongozi wa klabu hiyo utakapotangaza rasmi majina ya nyota watakaowaacha.

Wachezaji ambao wanatajwa kutokuwa sehemu ya timu hiyo kwa msimu ujao ni Mahlatsi Makudubela (Skudu), Joyce Lomalisa na Augustine Okrah. Kwa mujibu ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe kuanzia Julai Mosi mwaka huu, timu hiyo itaanza kuwatangaza wachezaji watakaoachana nao na wale wa kuongezewa mkataba.

Ameeleza sababu ya kuchelewa kutangaza wachezaji wanaowaacha ni mipango yao waliyojiwekea pamoja na  nyota wao wapya kuchelewa kupewa barua zao za kuachwa yaani release leter.

“Matarajio yetu ifikiapo Julai Mosi, mwaka huu tunatangaza wanaoachwa na wanaongezewa mikataba, kuna wachezaji tayari tumeshamalizana nao lakini bado hawajapewa barua kutoka klabu walizotoka za kumaliza mikataba yao”.

“Tumefanya usajili mkubwa sana kwa sababu malengo yetu ni kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri ndani na michuano ya Kimataifa kucheza fainali ya Afrika, inatulazimu kusajili wachezaji bora,” amesema Kamwe.

Kuhusu suala la deni na kupelekea kufungiwa kusajili na Shirikisho la Kimataifa la mpira wa miguu (FIFA ), Kamwe amesema hakuna kesi yoyote ambayo inawahusu klabu hiyo kwa sababu ameshamalizana na wachezaji walikuwa wakiidai Yanga.

“Wachezaji hao ni Mamadou Doumbia na Lazorous Kambole wote tumeshamalizana nao Juni 14, mwaka huu siku moja kabla dirisha kubwa la usajili kufungiliwa ilikuwa Juni 15, jana tumepokea Email kutoka Fifa ikitoa siku tano kukamilisha usajili wa Kambole kwenye system,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa suala la Okra litawekwa wazi muda utakapifika ikiwa ataendelea kusalia ndani ya kikosi au ataondoka na hiyo ni baada ya mapendekezo na mipango ya kocha Gamondi.

Okrah ambaye klabu Bechem United (Ghana) imeishtaki klabu ya Yanga FIFA kushundwa kulipa hesemu ya ada ya uhamisho wa nyota huyo.

Imeelezwa kuwa ada ya uhamisho ni dola za kimarekani 120,000 (zaidi ya Millioni 314 za Tanzania), Yanga imeripotiwa kulipa dola 20,000 (Mill 52,300,00) kwa qjili ya kupata ITC ya mchezaji hali hiyo bado wanadaiwa dola 100,000 sawa na Mill. 261,500,00.

Related Articles

Back to top button