Muziki

Rayvanny anatukumbusha kitu kuhusu maisha!

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, amewaachia mashabiki wake na gumzo mitandaoni baada ya kuchapisha picha yake ya zamani na kuambatanisha ujumbe wa kutia moyo kuhusu safari ya maisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliandika: “Ukifumba macho jione mwingine, sio yule yule wa jana!!! Kwa (On God) hakuna kinachoshindikana.”

Ujumbe huo umeonekana kugusa wengi, ukionesha namna ambavyo mafanikio yanahitaji juhudi, uvumilivu na imani.

Rayvanny, ambaye amewahi kupitia changamoto mbalimbali kabla ya kufikia mafanikio makubwa katika muziki, ameonyesha wazi kuwa mabadiliko chanya yanawezekana kwa yeyote anayethubutu kuota na kupambania ndoto zake.

Mashabiki na wadau wa burudani wameendelea kumpongeza kwa hatua aliyofikia, wakieleza kuwa yeye ni mfano bora wa kuigwa kwa vijana wanaotamani kufanikiwa katika tasnia ya muziki na maisha kwa ujumla.

Kauli yake imebeba ujumbe mzito: katika maisha hupaswi kukata tamaa, bali unapaswa kujiamini, kufanya kazi kwa bidii na kuamini kuwa hakuna lisilowezekana.

Related Articles

Back to top button