Rais Karume kufunga ZIFF 2024
ZANZIBAR: RAIS mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, leo usiku anatarajiwa kufunga Tamasha la 27 la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) lililofanyika kwa siku nne kuanzia Agosti 1.
Tuzo mbali mbali zitatolewa kwa washindi kutoka filamu 70 zinazoshindanishwa mwaka huu wa 2024.
Awali filamu 3,000 ziliwasilishwa ambapo filamu 70 ziliingia katika shindano hilo.
Licha ya kulifunga tamasha hilo, Rais mstaafu Karume atakabidhi tuzo kwa washindi na kutoa hotuba yake huku tuzo hizo zikitolewa kwa filamu kutoka mabara yote likiwemo Afrika, Ulaya, Asia na Marekani.
Tuzo hizo zimegawanyika katika makundi matatu. Tuzo za dhahabu, Tuzo maalumu na tuzo za tamthilia.
Tuzo za dhababu zitaenda kwa Filamu bora ya makala, Filamu bora ya Afrika Mashariki, filamu bora ya dokumentari, filamu bora ya vikaragosi, muigizaji bora wa kike wa Tanzania, muigizaji bora wa kiume wa Tanzania, muigizaji bora wa filamu wa kiume wa Afrika Mashariki na muigizaji bora wa filamu wa Afrika Mashariki wa Kike.
Pia kutakuwa na migizaji bora wa kike na kiume katika tamthilia na tamthilia bora.
Kundi jingine ni tuzo maalumu ambapo kutakuwa na tuzo ya Mwenyekiti, Tuzo ya maisha yaliyotukuka na tuzo ya Emerson Zanzibar.