Afrika Mashariki

Raila Odinga ahudhuria mazishi ya Fred Omondi

NAIROBI, Kenya: KIONGOZI wa Azimio na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amehudhuria ibada ya mazishi ya mchekeshaji Fred Omondi aliyefariki katika ajali ya gari.

Raila aliwasili leo asubuhi Sega, Bondo, Kaunti ya Siaya kwa helikopta, akiongozana na Gavana wa Siaya James Orengo pamoja na Kiongozi wa Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi.

Fred anazikwa katika nyumba ya familia yake katika Kaunti ya Siaya. Mwili wake ulisafirishwa kwa ndege kutoka Nairobi hadi Kisumu Ijumaa jioni kisha kusafirishwa kwa barabara hadi Sega.

Mazishi yanafanyika katika Shule ya Msingi ya Nyambiro. Watu mashuhuri waliofika kutoa rambirambi zao kwa familia ni pamoja na Mbunge Jalang’o, Tumbili, YY, Amber Ray, Ken Rapudo na Dufla na wengine wengi.

Fred amefariki na kuwaacha katika majonzi makubwa kaka yake mchekeshaji maarufu kenya nan je ya Kenya Eric Omondi na dada yake Irene Adhiambo.

Related Articles

Back to top button