Prezzo atangaza kugombea urais Kenya

MSANII maarufu wa hip hop kutoka Kenya, Jackson Ngechu maarufu kama Prezzo, ametangaza rasmi azma yake ya kuwania urais wa Kenya katika uchaguzi wa mwaka 2027 kupitia chama chake, CMB (Chama Mabadiliko Busara).
Prezzo amesema dhamira yake ni kuleta mabadiliko makubwa katika nchi na kuwa sauti ya vijana, akieleza kuwa anaamini wakati umefika kwa kizazi kipya kushika hatamu za uongozi.
Tangazo lake limezua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakisubiri kuona mwelekeo wake mpya wa kisiasa na jinsi atakavyoendesha kampeni zake.
Mbali na siasa, Prezzo pia amefunguka kuhusu maisha yake binafsi, akisema ameokoka na kumrudia Mungu, akiacha maisha ya zamani ili kuanza safari mpya yenye maadili na maono mapya.
Je, Prezzo anaweza kuleta mageuzi katika siasa za Kenya? Ni jambo la kusubiri na kuona.