Maignan apewa ruksa ya mazoezi

MILAN:Golikipa wa AC Milan Mike Maignan ameruhusiwa kuanza mazoezi ya kujiweka sawa kurejea uwanjani baada ya Mfaransa huyo mwenye miaka 29 kuonekana kupoteza fahamu kwa muda mfupi baada ya kugongana na beki wake Alex Jimenez kwenye mchezo wa Serie A walioshinda 4-0 mbele ya Udinese wikiendi iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo baadaye Jumanne ilieleza kuwa mchezaji huyo anaendelea vizuri na jumatano hii atarejea kuanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na michezo iliyosalia ya kikosi hicho kwa msimu huu.
“Leo Mike Maignan amefanya vipimo vya kitaalamu na madaktari wetu vipimo ambavyo vimeondoa hatari ya iliyokuwa ikimkabili na sasa yuko tayari kurejea mazoezini taratibu muda wowote kuanzia Jumatano” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ni ahueni kwa Mashabiki wa AC Milan ilio nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Serie A baada ya hali ya wasiwasi kutanda juu ya jeraha la kichwa la Maignan dakika ya 53 ya ambaye ni moja ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho kitakachokuwa wenyeji wa Atalanta ilio nafasi ya 3 Jumapili hii.