Mastaa

Paula bado nipo upande wa Marioo

DAR ES SALAAM:MZAZI mwenzake na Msanii Omary Mwanga Marioo Paula Paul amesema sababu ya kuingilia ugomvi kati ya mpenzi wake na Ibra, aliingilia ugomvi huo akimtaja Ibraah kuacha kabisa kumzungumzia vibaya Marioo.

Paula amesema
“Kwangu ni lazima kuingilia ugomvi au changamoto yoyote inayomtokea mpenzi wangu au baba wa mtoto wangu.

“Sipendi kumuona akishambuliwa mitandaoni halafu mimi nikakaa kimya,” amesema Paula.

Ameeleza kuwa pia hapendi tabia ya watu kudhalilishana kupitia mitandao ya kijamii, akisema mambo yanayochapishwa huko yanaweza kuhifadhiwa na kuendelea kuonekana hata baada ya tukio kupita.

“Mimi sipendi mambo ya kudhalilishana mitandaoni kwa sababu mambo yanayowekwa huko yanahifadhiwa.

“Pia nina mtoto, hivyo ni lazima nifikirie mambo haya,” amesema.

Related Articles

Back to top button