Mastaa

Wokovu wamweka mbali ‘staa’ wa juakali

DAR ES SALAAM: MSANII anayetamba katika tamthilia ya Juakali Godliver Gordian, ameweka wazi sababu ya kutohudhuli sherehe za wasanii wenzake.

Akizungumza na SpotiLeo, Godliver amesema baada ya kumrudia Mungu ameona maeneo pekee yanayompendeza kwenda tofauti na kwenye mikusanyiko ya ibada ni kutulia nyumbani kwake muda mwingi akifanya maombi.

“Nimejiwekea mipaka yangu ya maombi na sala ndiyo maana nakosa muda wa kuhudhuria shughuli za wasanii wezangu,” alisema.

Kwa sasa amesema amejiwekea kwa Mungu na hawezi kufanya lolote bila kumshirikisha Mungu wake kwa sala na maombi.

Related Articles

Back to top button